Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Maji Prof. Mark Mwandosya wakati alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa kusanyiko la kwanza la uwekezaji katika Bonde la Ziwa Victoria lililofanyika jijini Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wawekezaji kutoka katika nchi za Afrika Mashariki.
Mwandosya amezitaja changamoto zinazochangia kuwepo kwa hali hiyo ni pamoja na umaskini, migogoro ya kiuchumi, ukosefu wa raslimali watu matumizi mabaya ya vyanzo vya maji , uchafuzi mazingira na ukuaji wa kasi ya ongezeko la watu.
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Hafsa Mossi amesema kuwa kutokana na raslimali zilizo katika Bonde la Ziwa Victoria, ana imani kuwa wawekezaji wenye sifa watajitokeza kuja kuwekeza kwa lengo la kuwaondolea umaskini wakai wanaozunguka bonde hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.