ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 18, 2018

HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA YAOKOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 150 ZILIZOKUWA ZIKIINGIA KWENYE MIFUKO YA WAJANJA KILA MWEZI


GSENGOtV

Baada ya kudhibiti mianya ya kupiga fedha, mchezo unaosemekana ulikuwa ukifanywa na baadhi ya wahudumu na viongozi wasio waaminifu, wakitafuna fedha za mapato ndani ya hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure, hatimaye hospitali hiyo imefanikiwa kukomboa zaidi ya shilingi milioni 150 kwenye makusanyo ya kila mwezi, fedha zilizokuwa zikiliwa na wajanja wachache.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella wakati akipokea msaada wa vitanda 40 na magodoro yake, uliotolewa na Exim Bank kama mwendelezo wa kampeni ya benki hiyo kurejesha sehemu ya faida kwa jamii.

Kupitia ripoti ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Sekou Toure, Dr. Rutachunzibwa Thoma, aliyoipenyeza kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, inaonesha kwa sasa hospitali hiyo inakusanya wastani wa shilingi za Tanzania milioni 200, kwa mwezi ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo ilikuwa ikikusanya milioni 40 hadi 50 tu kwa mwezi.


 Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Sekou Toure, Dr. Rutachunzibwa
 Sehemu ya waganga, wauguzi, wasaidizi na viongozi Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure
 Sehemu ya waganga, wauguzi, wasaidizi na viongozi Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure
 Sehemu ya waganga, wauguzi, wasaidizi na viongozi Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure
 Watu na taaluma zao.
Benki ya Exim imetoa msaada wa vitanda na magodoro 40 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni muendelezo wa kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.
Hospitali hiyo ya Sekou Toure imekuwa ya kumi kupokea msaada baada ya Hospitali nyingine za mikoa mbalimbali hapa nchini kunufaika na mapango huo wenye lengo la kutoa vitanda na magodoro 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.