ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 16, 2018

DAR ES SALAAM KUMEKUCHA, RAIS MAGUFULI ASHUSHA NEEMA.*

 Na Zephania Mandia wa G.sengo TV.

Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam wameendelea kula Matunda ya serikali ya awamu ya tano baada ya Rais Dr. John Magufuli kutoa zaidi Shilingi Billion 250 kwaajili ya utekelezaji wa Miradi Mkakati ya kuziwezesha Halmashauri za jiji hilo kujiendesha zenyewe ili kupunguza utegemezi wa fedha kutoka Serikali kuu. 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema miongoni mwa miradi itakayotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha kisasa cha Mabasi ya Mikoani Mbezi Luis kitakachogharimu zaidi ya shilingi Billion 50 ambacho ujenzi wake utaanza Mwezi June na kuchukuwa miezi 18 kukamilika. 

RC Makonda amesema jengo hilo litakuwa na gorofa tano ambapo kituo hicho cha kisasa kitakuwa na uwezo wa kuchukuwa Mabasi 200 na Maegesho magari 300 (Underground parking) ambapo ndani kituo kutakuwa na huduma zote muhimu ikiwemo Hotel, Hostel, Shopping Mall,Maduka, Migahawa, sehemu za mapumziko, Kituo cha Polisi, Bustani, Bank, Vyoo vya kisasa pamoja na Ofisi za kampuni za Magari.



 Aidha RC Makonda amesema miradi mingine ni Ujenzi wa Soko la kisasa Kisutu litakalogharimu shilingi Billion 16, Kituo cha Mabasi Chamanzi Mkondogwa, Ujenzi wa Machinjio ya kisasa Vingunguti yenye thamani ya Billion 8.5 itakayokuwa na uwezo wa kuchinja Ng'ombe 1,000 kwa siku hali itakayoondoa uagizwaji wa Nyama Nje ya nchi kwaajili ya kuuzwa kwenye Hotel na Supermarket ambapo kukamikika kwa mradi huu utawezesha wazawa kupata soko la nyama la uhakika, Ujenzi wa Soko la Mburahati Billion Billion 2.7 kituo cha Daladala Tuangoma, Soko la Kibada Billion 14 pamoja na miradi mingine mingi ikiwemo Fukwe za Coco, Ujenzi wa Shopping Mall na miradi mingine lukuki inayofanywa na Rais Magufuli kwenye Mkoa wa Dar es salaam.





RC Makonda amemshukuru Rais Magufuli kwa kwa dhamira njema ya kusaidia kutatua kero za wananchi ambapo amewasihi wananchi wa Dar es salaam kukaa mkao wa kula kwa kuchangamkia fursa za ajira zitakazotolewa kwenye miradi hiyo. 

HUU NI UPENDO WA DHATI WA RAIS MAGUFULI KWA  WANANCHI WAKE.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.