ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 18, 2018

SERIKALI KUTOA MASHINE ZA EFD KWA WAFANYABIASHARA WADOGO KUANZIA JULAI MOSI

Serikali imesema kuanzia Julai mosi mwaka huu, kupitia Mamlaka ya Mapato nchini- TRA itaanza kutoa mashine za risiti za kielektroniki-EFD kwa wafanyabiashara wadogo nchi nzima.
Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Nsimbo, Richard Mbogo aliyeishauri serikali kutoa mashine za EFD bure kwa wafanyabiashara wadogo.
“Tumeanza utaratibu wa kufikia wafanyabiashara wote, na hata kwanza mashine hizo hazikutolewa bure wafanyabiashara wakubwa walipewa kwa mkopo, kwa hivyo tuna mpango kupitia TRA ifikapo Julai 1, 2018 kutoa mashine hizo kwa wafanyabiashara wadogo,” amesema.
Amesema awamu hii serikali itaacha kutumia mawakala katika kugawa mashine hizo ili kuondoa mzigo wa bei kwa wafanyabiashara wadogo.
“TRA itaanza kutoa yenyewe mashine hizi na kuacha kutumia mawakala kitendo kilichoongeza gharama. TRA ikianza kutoa ghrama zitapungua,” amesema Dkt. Kijaji.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.