ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 21, 2011

MZOZO JUU YA MAZISHI YA GADDAFI.

Mazishi ya Kanali Gaddafi yamesitishwa kutokana na tofauti zilizozuka baina ya maafisa wa Libya kuhusu jinsi ya kufanya maziko hayo.
Chini ya utamaduni wa Kiislam, maziko hutakiwa kufanyika haraka iwezekanavyo. Lakini waziri wa mafuta wa Libya amesema mwili wa Gaddafi huenda ukahifadhiwa "kwa siku kadhaa".

Haifahamiki kama kiongozi huyo wa zamani atazikwa Sirte, mji aliouawa siku ya Alhamis, au Misrata, mji aliopelekwa baada ya kufa, au mahala pengine.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amesema kifo cha Muammar Gaddafi kinamaanisha shughuli za Nato nchini Libya zimefikia kikomo.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa mamlaka nchini Libya zinafanya mipango ya kufanya mazishi ya siri kwa kiongozi huyo. Hata hivyo, inaonekana huenda kukawa na kuchelewa kufanyika kwa mazishi hayo, ambayo chini ya utamaduni wa Kiislam mazishi hufanyika haraka iwezekanavyo.

Waziri wa mafuta Ali Tarhouni aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa mwili wa Kanali Gaddafi huenda ukahifhadhiwa "kwa siku kadhaa".

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.