Timu ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa,iliyokuwa inachunguza kiini cha kuuwa walinzi wa amani 15 wa Tanzania huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwishoni mwa mwaka jana,imesema tukio hilo linadhihirisha “mapungufu” ya jinsi gani askari wa Umoja huo wanavyopatiwa mafunzo.
Ikiwasilisha ripoti yao hapo jana, timu ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa ilisema imegundua mapungufu pia kwenye mfumo wa utoaji amri, uongozi pamoja na ukosefu wa vikosi vya uwezeshaji kama vile vya anga, wahandisi na ujasusi.
Katika shambulio hilo la Desemba 7 kwenye mji wa Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini, wanajeshi 15 wa Tanzania waliuawa na wengine 43 kujeruhiwa katika tukio linalotajwa kuwa baya zaidi kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa kilichopelekwa nchini DRC tangu mwaka 1999.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, waasi wa jeshi la ADF la nchini Uganda ndio waliohusika na shambulio hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.