Straika wa klabu ya Manchester United, Romelu Lukaku amejiunga na Roc Nation Sports iliyopo chini ya kampuni ya Roc Nation inayomilikiwa na msanii wa muziki nchini Marekani, Jay-Z.
Nyota huyo wa Man United, Lukaku ameposti picha katika mitandao yake ya kijamii zinazomuonyesha akikaribishwa katika familia hiyo ya michezo huko New York.
Jay-Z alianzisha kampuni ya Roc Nation kwaajili ya burudani kabla ya kutanua wigo zaidi hadi kufikia Roc Nation Sports na Lukaku kuwa mchezaji wa kwanza kujiunga kutoka ligi kuu ya Uingereza.
Roc Nation Sports ni sehemu ya kampuni ya Roc Nation ambayo imeanzishwa na Jay – Z mwaka 2013 kwa kushirikiana na Shirika la kukuza vipaji vya michezo (Creative Artists Agency) huku ikiwa na lengo la kuenua na kukuza vipaji huko Los Angeles na California.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anakuwa wa pili kwa upande wa mchezo wa mpira wa miguu baada ya beki wa Bayern Munich, Jerome Boateng kujiunga na familia hiyo yenye maskani yake nchini Marekani.
KUHUSU 'ROC NATION SPORTS'
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.