ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 29, 2012

ILALA NA KINONDONI KESHO KUONYESHANA UBABE FAINALI SAFARI LAGER POOL TAIFA ZINAZOFANYIKA MWANZA.

 Mashindano ya Safari Pool Taifa ambapo jiji la Mwanza kwa mara ya kwanza mwaka huu 2012  limepewa hadhi ya kuwa wenyeji yamefikia hatua ya fainali ambapo kesho jumapili washindi mmoja mmoja yaani Single kwa wanaume na wanawake na mshindi kwa timu watapatikana na kwenda kuzawadiwa medali zao na vitita vyao. 


 Mashindano hayo yaliyoshirikisha timu 16 za mikoa mbalimbali hapa nchini yameshuhudia wenyeji Mwanza wakitolewa kiulaini kwenye hatua za makundi na kuziacha timu za  Dar es salaam,  ziking'ara kwa kuzisambaratisha timu za vilabu toka mikoa mingine kwa makundi hatimaye Kinondoni na Ilala zimefanikiwa kutinga fainali.

Kinondoni imetinga fainali mara baada ya kupata ushindi dhidi ya Morogoro kwa fame 13-10, nayo timu ya Kayumba kutoka Ilala wao wametinga fainali kwa kuinyuka Arusha kwa fame 13-9.


Kwa upande wa Mchezaji mmoja mmoja yaani Single Safari Lager Pool Taifa Wanawake:- Cecilia Kileo wa Kilimanjaro ameingia fainali ambaye atacheza na Betty Sanga wa Mbeya. Kwa upande wa Wanaume:- Solomon Elias kutoka Mbeya ameingia fainali akitarajia kucheza na Athumani Selemani.

Mgeni rasmi katika kufunga Fainali za Safari Lager Pool Taifa hiyo kesho jumapili katika jiji la mwanza ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari na utamaduni Leonard Thadeo.
Wadau wakifuatilia kwa makini moja ya michezo ya nusu fainali ya Safari Lager Pool inayofanyika Monarch Holel wilayani Ilemela jijini Mwanza.

 Mchezaji kutoka timu ya mkoa wa Arusha Fayu Stanley akisukuma kipira kwenye mcchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu na matokeo Arusha wameinyakuwa nafasi hiyo kwa kuikandamiza Morogoro fame 13-8. 


Aliy Said Aboubakari (kushoto) ambaye ni shabiki mkuu wa Kayumba 'Yeyo' toka Ilala jijini Dar es salaam akishow love na Team Captain wa Kayumba pool club Emanuel Loya.
Sikiliza majigambo ya Ilala na Temekekuelekea fainali ya Safari Lager Pool hapo kesho.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.