ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 28, 2012

BREAKING NEWS: CCM YAREJESHA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA KWA KUSHINDA UMEYA NA NAIBU MEYA, NAO UCHAGUZI WA ILEMELA WAAHIRISHWA KUTOKANA NA PINGAMIZI LA MATATA

Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula kupitia CCM (katikati) akiwa na Naibu Meya John Minja (CCM) wakitambulishwa na Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe baada ya kutangazwa washindi  kufuatia uchaguzi uliofanyika leo katika ukumbi wa halmashauri ya jiji la Mwanza.

 Kikao cha Uchaguzi cha Halmashauri ya Manispaa ya Nyamagana jijini Mwanza kimemchagua diwani wa Kata ya Mkolani Mh. Stanslaus Mabula wa CCM kuwa Meya wa jiji hilo mara baada ya kumshinda mshindani wake Charles Chinchibela wa CHADEMA aliyepata kura 8 ile hali Mabula akipata kura 11.

Ni picha ya pamoja Meya Mabula, mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga(katikati) na Naibu meya John Minja wakiwa katika ofisi ya Mstahiki Meya 


Diwani wa kata ya Kitangili Henry Matata (aliyevuliwa uanachama CHADEMA) akisalimiana na diwani mwenzake Marietha Chenyenge huku mkononi akiwa na hati ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza iliyozuia kufanyika wa Meya na Naibu Meya mpaka pale kesi iliyofunguliwa na diwani huyo kupinga CHADEMA kuteua wagombea wa nafasi hizo, kwa chati  mbunge wa jimbo la Ilemela Highness Kiwia (aliyesimama) akiwa bize na simu yake ya kiganjani, kabla ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa Manispaa ya Ilemela.
Ikumbukwe kuwa leo kulikuwa na chaguzi mbili za Ma- Meya na Ma- Naibu wake wa Halmashauri ya jiji la Mwanza (Nyamagana) na Manispaa ya Ilemela, baada ya uchaguzi wa Nyamagana kumalizika na wajumbe wake kuondoka ukumbini  ili kuwapisha wajumbe wa wilaya ya Ilemela, nao waliketi katika ukumbi wa uchaguzi wakisubiri kushiriki uchaguzi wa kuteuwa Meya na Naibu Meya wao ambapo uchaguzi huo haukufanyika kufuatia diwani wa kata ya Kitangili kufungua kesi katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kupinga kuvuliwa uanachama, kupinga kuenguliwa katika mchakato wa kuwania nafasi ya Meya hadi hapo uamuzi wa kesi yake utakapo tolewa, kutokana na kuwa na hati ya Mahakama inayomruhusu aidha kuruhusiwa kushiriki kupitia chama chake cha zamani (CHADEMA) au chama chake kutofanya uteuzi wa wagombea.

Aliyekuwa mgombea nafasi ya Meya wa Manispaa ya Ilemela Abubakar Kapera diwani kata ya Nyamanoro (kulia)   na kushoto kwake ni diwani wa kata ya Kirumba Danny Kahungu aliyekuwa akiwania nafasi ya Naibu Meya Ilemela  wote kutoka CHADEMA ndani ya ukumbi wa uchaguzi kabla ya uchaguzi wao kuahirishwa kutokana na zuio.

Kutoka kushoto ni aliyekuwa Meya wa jiji la Mwanza kabla ya jiji hilo kugawanywa kuwa Manispaa na Halmashauri, diwani Manyarere akiwa na diwani Rose Brown na diwani wa viti maalum ndani ya ukumbi wa Uchaguzi kutafuta Meya na Naibu wake Nyamagana.

Madiwani wa CCM wilaya ya ilemela kabla ya uchaguzi wao kuahirishwa.

Madiwani wa CHADEMA wakiwa na mbunge wao  wa wilaya ya Ilemela Highness Kiwia (katikati) wakisubiri taratibu za uchaguzi ambao hata hivyo haukufanyika.

Meya wa jiji la Mwanza (wa3kutoka kushoto) Naibu Meya (wa kwanza kushoto) wakiwa pamoja na Madiwani wa CCM wakimsikiliza mbunge wa viti maalum Maria Hewa (wa pili kutoka kulia) aliyekuwa akisema "Chama kimerudisha heshima yake katika jiji la Mwanza"
MAPOKEZI MAKAO MAKUU YA CHAMA MWANZA...
Nje ya ofisi za CCM kulikuwa na makaribisho ya kutosha kwa wanachama mbalimbali kujitokeza kumlaki Meya mpya na naibu wake.

Meya na naibu wake wakiwasili .....

Shangwe zikatawala kwa mtu wao...

Ni full raha, ni full kujiachia kwa wanachama wa CCM Nyamagana jijini Mwanza.

Hapa Meya aklikutana na Mwenyekiti wa Vijana mkoa wa Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.