ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 28, 2012

TANZANIA INVESTMENT BANK LIMITED (TIB) YAFUNGUA TAWI LAKE LA KANDA YA ZIWA: MWANZA. KUWA KITOVU

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo (mwenye suti ya brown) akifungua rasmi tawi la Tanzania Investment Bank (TIB) mkoani mwake shughuli iliyofanyika leo mchana katika ofisi za huduma za benki hiyo zilizopo ndani ya jengo la PPF Plaza jijini Mwanza.


Hii ndiyo  Benki ya Uwekezaji raslimali nchini Tanzania (TIB)

The inshu..


Mara baada ya kutambulishwa huduma za kibenki zitolewazo na TIB Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo alihamasika kufungua akaunti kama inavyoonekana pichani.


Waalikwa na viongozi kwenye uzinduzi huo. 


Ngoma asili ilihusishwa...


Sehemu ya wadau waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo..


Benki ya TIB tawi la Mwanza itawanufaisha wateja wa mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Simiyu, Kigoma, Mara na Mwanza huku ikiendelea kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu  ambapo imelenga kutoa mikopo ya shilingi bilioni 1,099 kufikia mwaka 2015 ili wananchi wajikwamuwe toka lindi la umaskini.


Wafanyakazi wa Tanzania Investment Bank.


Mkurugenzi mwendeshaji wa Benki ya TIB Bw. Peter Noni ameiomba serikali kuongeza mtaji katika benki hiyo ili iweze kukidhi mahitaji ya wateja ambao mahitaji yao ni makubwa. 


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akihutubia wananchi ndani ya uzinduzi huo..


Mc wa Uzinduzi huo Ephraim Kibonde wa Jahazi Clouds Fm hapa alitupa kibonzo kwa meza kuu watu....Kwa-kwa-kwa!!


Zawadi kwa mkuu wa mkoa toka benki ya TIB.


Akina dada wateja wa TIB walio alikwakwenye uzinduzi huo.


Picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, wafanyakazi wa TIB, uongozi na wageni viongozi meza kuu. 



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.