Emanuel Mgaya aka Masanja Mkandamizaji akizungumza na kusanyiko lililojitokeza kwenye mazishi ya Askofu wa EAGT hayati Moses Kulola aliyefariki na kuzikwa kwenye eneo la wiwanja vya kanisa la EAGT Bugando jijini Mwanza.
Mbali ya kuwa mchekeshaji mahiri, Masanja Mkandamizaji ana karama ya uinjilisti, akitambulika kama Mchungaji wa kanisa la Mito ya Baraka. Katika mazishi ya Askofu kulola, Masanja alipata nafasi ya kuimba (kwani ana album ya muziki wa Injili) katika ufafanuzi wa moja ya nyimbo zake alisema "Hakuna mstari kwenye Biblia usemao 'baada ya kifo ni kesi', bali kuna unaosema 'baada ya kifo ni hukumu'," Kisha akaongeza... "Kuna tofauti kati ya kesi na hukumu, kesi unasomewa na kujitetea na mengineyo ya kutafuta ushahidi, lakini hukumu ni kwamba mambo yoooote yamejulikana na sasa kinachobakia ni kusalimika ukarejea uraiani au kukutana na kifungo"
"Ingekuwa baada ya kifo ni kesi hakuna Mtanzania angeenda motoni kwani Watanzania ni mafundi kwenye kujitetea hivyo Mungu aliliona hilo....."(Bofya play kumsikiliza.)
Taarifa kwa Umma Kuhusu Ongezeko la Bei za Mafuta.
-
Dar es Salaam, Tanzania
Tunatambua ongezeko kubwa la hivi karibuni la bei za mafuta ambalo
limeongezeka kwa asilimia 33. Kama jukwaa linalolenga kusawaz...
Serikali Yaongeza Muda wa Tume ya Uchunguzi
-
*Na Mwandishi Wetu*
*DODOMA, Aprili 4, 2026 — Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
imetangaza kuongeza muda wa kukamilisha kazi kwa Tume ya Kuchun...
0 comments:
Post a Comment