ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 28, 2017

MTO MIRONGO WAFUNGUKA LEO BAADA YA ZAIDI MIAKA TISA

NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGOBLOG TV.


Ongezeko la idadi ya watu katika sehemu za mijini imekuwa chanzo kikubwa cha uzalishaji wa taka kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu zinazofanywa katika maeneo hayo hivyo kupelekea gharama kubwa ya usafishaji KIOMONI KIBAMBA kurugenzi wa jiji la mwanza amesema mto huo unazaidi ya miaka tisa bila kufanyiwa usafimkubwa kama huo.


Ikiwa ni muda mchache kufikia majira ya mvua za masika mkurugenzi wa Jiji la Mwanza KIOMONI KIBAMABA ameanza jitihada za kusafisha maeneo korofi ya jiji la Mwanza kwa kuanza na Mto Mirongo uliyopo katikati ya jiji la Mwanza.


Takataka pamoja na mchanga unaotoka katika maeneo mbalimbal za jiji la Mwanza hupitia katika mto Mirongo ambao humwaga maji yake katikaziwa victoria.


Mkuruenzi wa jiji la Mwanza KIOMONI KIBAMBA anasema ameamua kuwa mfano wa kusafisha mto huu ili kuepukana na madhara mafuriko yanayosababishwa na uchafu unaopita katika mtoa huo.


Wananchi mbalimbali walioshuhudia mto huo ukisafishwa waliipongeza halamahuri ya jiji mwanza kwa kusafisha mto huo ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa na madhara kwao.


Kila mwezi jiji hilo ulipa milioni 250 kwa ajili Usafi wa mazingira wa jiji la mwanza hivyo kufanya  eneo hilo kuchukua kiasi kikuwa cha mapato ya jiji hilo kwa kuwalipa watendaji na kampuni zinazo jihusisha na usafi w jiji hilo,G.SENGO TV imefika katika mto huo nakushudia mkurugenzi KIOMONI KIBAMBA akisaidiana na watendajiwake kuhakikisha mto huo unafungunguka maramoja kabla ya mvua za masika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.