Wadudu na wanyama wakali kama mamba, nyoka, kasa, chatu hata nyani wa msituni huishi kwenye magugu haya yaliyo changanyika na magugu aina ya matende.
Taswira hii imetanda kwa takribani siku 3 hadi hii leo ambapo imehama na kuelekea upande wa pili wa fukwe na kujikita.
Pamoja na kuwa na faida kama sura ya Utalii pia magugu haya yanasifika kama chanzo cha mazalia ya samaki wa aina mbalimbali.
Moja kati ya athari kubwa inayojitokeza pindi magugu haya yanapotanda ni pale yanapoathiri shughuli za usafiri na usafirishaji kwani hukinga njia za boti na meli zinazosafiri ziwani, ilitokea mwaka 2015 eneo la Kigongo wilayani Misungwi mkoani Mwanza kiasi cha kutatiza shughuli za usafiri na usafirishaji ambapo zaidi ya magari 200 ya mizigo yalikwama kusafiri katika eneo la Kigongo na Busisi na kuleta athari kubwa kwa wananchi, wafanyabiashara na wasaka huduma.
Magugu maji yalitanda ziwa Victoria eneo la kivuko hicho kwa ukubwa kwa hekari nne na kusababisha vivuko kutofanya kazi.
Mbele ya ghati ya Jembe Boat.
Kwa wale wananchi wanaoteka maji, kuoga, kufua au kufanya shughuli zozote za kijamii kando kando mwa ziwa Victoria huwa hatarini kuliwa na mamba + nyoka wanaoweka makazi yao chini na ndani ya magugu maji....
Habari iliyosikikika katika #KAZINANGOMA @mansourjumanne @gsengo @djscorpion
Kutoka upande wa pili na muonekano wa Mbele ya ghati ya Jembe Boat na Jembe Beach uliofichwa na magugu hayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.