Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wapili kushoto) akitoa maagizo kwa uongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania leo Jijini Dar es Salaam ya kutoa elimu kwa wadau wa tasnia ya filamu kuzingatia maadili ya kitaaluma wapoigiza kulingana taaluma mbalimbali ilikuzipa kazi zao mvuto, (watatu kulia) ni Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo.
Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo (wa kwanza kulia) akimweleza Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa kwanza kushoto) mpango wa bodi kuwa na pragramu ya kuanzisha filamu bora ya mwezi itakayooneshwa kwa siku moja katika kumbi za sinema kote nchini leo alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kupata taarifa za uendeshaji wa shughuli taasisi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo (wa kwanza kushoto) akitoa ushauri kwa Bodi ya Filamu Tanzania kutumia tovuti yake wakati wa kutangaza filamu bora ya mwezi ili kutangaza tovuti hiyo mbele ya Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wapili kushoto) leo jijini Dar es Salaam katika kikao cha ufuatiliaji wa shughuli za bodi.
Afisa Maendeleo ya Filamu kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw.Simon Peter akitoa taarifa ya utekelezaji na majukumu ya Kitengo cha Maendeleo ya kazi za Filamu mbele ya Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam katika kikao cha ufuatiliaji wa shughuli za bodi.
Kaimu Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa kwanza
kushoto) akizungumza mara baada ya kikao
cha ufuatiliaji wa shughuli za Bodi ya Filamu Tanznia leo jijini Dar es
Salaam na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo (wa kwanza kulia) pamoja na Kaimu
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo (wa pili kulia).
Bodi
ya Filamu Tanzania toeni elimu ya Maadili ya Kitaaluma kwa Wasanii
Na Anitha Jonas –
WHUSM,Dar es Salaam
29/12/2019
Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi amegiza uongozi wa
Bodi ya Filamu Tanzania kuhakikisha unatoa mafunzo kwa wadau wa tasnia ya
filamu katika kuzingatia maadili ya kitaaluma.
Dkt.Possi ametoa
agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam alipotembelea Ofisi za Bodi ya Filamu
Tanzania kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa shughuli zao pamoja na uandaaji
wa Marekebisho ya Kanuni za Sheria ya
Bodi ya Filamu na Michezo yakuigiza.
“Kumekuwa na changamoto
kubwa kwa baadhi ya kazi za filamu kukosa uhalisia katika maigizo ya kitaaluma haswa
pale wanapoigiza kuhusu taaluma mbalimbali mfano Madaktari,Wanasheria au Wahandisi na hii
inapelekea kupoteza mvuto wa filamu hizo,”alisema Dkt.Possi.
Akiendelea kuzungumza
Dkt.Possi alisistiza kuwa bodi inapashwa kuandaa mradi utakaosaidia wadau
watasnia hiyo kupata elimu na pia kuipaisha tasnia hiyo katika nyanja
mbalimbali ikiwemo ngazi za kimataifa na
kuimarisha uandaaji wa kazi hizo kwa kuwa na viwango vyenye ubora.
Nae Kaimu Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Dkt.Kiagho Kilonzo alisema kuwa Bodi inampango wa
kuanzisha programu ya kuwa na filamu ya
mwezi ya kitanzania ambapo filamu hiyo itapigiwa kura na watanzania na baada ya
kushinda itazinduliwa katika Majumba ya Sinema nchini na kwenye vingamuzi
kadhaa nchi nzima na kuonyeshwa siku moja katika muda mmoja lengo ikiwa ni
kuzitafutia masoko filamu za kitanzania na kukuza kipato cha wanatasnia wa
filamu.
“Bodi inampango wa
Kuanzisha Kanzi Data ya Waandaji wa kazi za
Filamu,Wasambazaji,Waigizaji,Waongozaji na Waandishi wa Miswada ya Filamu lengo
likiwa kupata takwimu zao, ili kuwa na njia rahisi ya kuweza kuwasaidia kiuchumi
wadau hawa ili angalau waweze kupata bima ya afya au kuwasaidia kupata
mikopo,”alisema Dkt.Kilonzo.
Pamoja na hayo nae
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo aliishauri
Bodi kutumia tovuti yake katika kipindi cha kupigia kura filamu bora ya
mwezi ili kuweza kuitangaza tovuti hiyo kwa wananchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.