ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 30, 2019

MCHEZAJI WA YANGA ATAKAYEFANYA VIZURI MECHI DHIDI YA SIMBA KUCHOMOKA NA ZAWADI NONO TOKA GSM


Kuelekea mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi, Kampuni ya GSM Group, ambao ni moja ya wadhamini wa Yanga inatarajia kutoa zawadi ya godoro kwa mchezaji wa klabu hiyo atakayeibuka nyota wa mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari  Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM Group, Matina Nkurlu, alisema wameamua kutoa zawadi hiyo ili kuwapa morari wachezaji wa Yanga.

Alisema wao kama wadhamini wa Yanga ni wajibu wao kuhakikisha timu hiyo inawapa raha mashabiki wake kwa kushinda mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla.

"Kuelekea mechi ya kukata na shoka kati ya watani wa jadi, Simba na Yanga, moja ya wadhamini wakuu wa timu ya Yanga, GSM Group kupitia godoro chapa GSM, tutatoa zawadi nono kwa mchezaji bora wa timu ya Yanga wakati wa mechi Yanga  na Simba kwa  kumzawadia godoro la nchi 5x6x8," alisema.

Aliendelea kwa kusema, "Tunaamini zawadi hii itawaongezea wachezaji morali ya kupambana kuiwezesha Yanga kupata ushindi na hivyo kuwapa raha mashabiki wao na kuendelea kupata matokeo chanya kwa mechi zingine zijazo,".

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.