ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 16, 2018

UFARANSA YAANZA KWA NEEMA KOMBE LA DUNIA.


GSENGOtV
Ufaransa imefanikiwa kuibuka na ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu nchini Russia wa mabao 2-1 dhidi ya Australia.

Mabao ya mchezo huo yametiwa kimiani na Antoine Griezmann katika dakika ya 58 kwa njia ya mkwaju wa penati na la pili likitiwa kimiani na Paul Pogba (80').

Bao pekee la Australia liliwekwa wavuni na Mile Jedinak mnamo dakika ya 62 kwa mkwaju wa penati.

Mechi hii imekuwa ya kwanza kushuhudiwa penati mbili ndani ya dakika 90 zikipigwa kwa pande zote.



Ushindi huu wa Ufaransa unawapa alama tatu muhimu kwenye kundi C ambapo baadaye Peru na Denmark watakuwa wanacheza pia kutoka kundi hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.