Afya, Kilimo, Elimu, Maji na Viwanda vimetajwa kama vipaumbele vitano kwenye bajeti mbadala ya mwaka wa fedha wa 2017/18 kutoka kwenye kambi rasmi ya upinzani bungeni.
Hayo yamesemwa na Kiongozi Mkuu wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe ambaye amesema licha ya baadhi ya bidhaa kuendelea kubaki katika bei yake ileile lakini bado ameikosoa akisema haitekelezeki huku akisema serikali imekuwa haizingatii sheria ya fedha na kiasi kinachotengwa kimekuwa hakitoshelezi matumizi ya wizara husika.
" Unajua hivyo vipaumbele vitano ambavyo sisi tumeviainisha ndivyo ambavyo vimekuwa vikiendana na maisha halisi ya mtanzania wa kawaida na siyo miradi mikubwa ambayo haimgusi mwananchi mmoja mmoja.
" Mfano wamekuwa wakiangaika kuutaja mradi wa Stigler's Geoge ambao umegharimu bilioni 700 fedha ambazo zingeingia kwenye mahitaji ya mwananchi mmoja mmoja kama elimu, maji na kilimo yangepunguza ukwasi wa maisha na kuongeza maendeleo zaidi," amesema Mbowe.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.