Awali nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba alikosa penati ambayo ingeipa ushindi kabla ya kumalizika kwa dakika 90 za kawaida.
Ivory Coast wamekosa penati 2 kati ya walizopiga ambapo Kolo Toure na Gervinho walikosa mikwaju hiyo.
Ivory Coast wataendelea kusubiri kunyakua kombe hilo, licha ya kuwa na wachezaji kadhaa wanaocheza Ulaya hasa katika Ligi Kuu ya England.
Tembo wa Ivory Coast walipoteza katika mchezo wa fainali mwaka 2006 dhidi ya Misri kwa mikwaju ya penati.
Lakini kwa Chipolopolo, ambao wamewahi kushika nafasi ya pili mara mbili, wamemaliza kwa ushindi kwa kuhanikizwa na vifo vya wachezaji wenzao mwaka 1993, baada ya ndege yao kuanguka karibu na uwanja ilipochezewa fainali mjini Libreville.
Mara ya mwisho kwa timu hiyo kutoka Kusini mwa Afrika kufika fainali ilikuwa mwaka 1994, mwaka mmoja tu baada ya wachezaji 18 wa nchi hiyo kupata ajali ya ndege karibu na mji mkuu wa Gabon.
Wakielekea katika mchezo wa fainali, wachezaji hao wa sasa walisema wanahisi nguvu kutokana na kukumbuka janga lililowapata wenzao.
Kwa kushinda mchezo wa fainali, wameonesha dhamira ya kuwashinda wapinzani wao ambao walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kupata ushindi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.