ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 22, 2012

KUTOKA KWA MDAU: KCMC HAWANA TENA KITENGO CHA TIBA KWA MOYO.

Albert,
Salam.

Pongezi kwa first born wako kutimiza miaka 7.

Sasa, baada ya kusoma taarifa ya msaada kwa Yvona, niliiweka pia wavuti.com ambapo mtu mmoja aliisoma kupitia twitter na kushauri mtoto apelekwe Muhimbili kwa kuwa KCMC haina tena kitengo kinachohusika na matatizo ya moyo.

Nikawasiliana na daktari ambaye alinifahamisha kuwa ni kweli daktari aliyekuwa anahusika na kitengo hicho KCMC hayupo tena.

Daktari huyu ameshauri mtoto apelekwe Bugando na siyo Muhimbili kwa kuwa Bugando ndiyo wana kitengo hicho. Yeye mwenyewe alifanya kazi Bugando kwa muda na ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Muhimbili hivyo anazifahamu hospitali zote mbili, pia ni mzaliwa wa Kilimanjaro hivyo anao marafiki na anafahamiana na wahusika wa KCMC.
Kwa sasa yupo nje, Japan, masomoni.

---------- message ----------
From: Subi <subi@wavuti.com>

Blogu hii inaahidi kuliwasilisha kwa mzazi, na kuomba wadau waendelee kumsaidia mtoto huyu kwa kuwasiliana na baba wa mtoto kupitia 0754 724278 au 0782 946177

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.