Simba imewasili leo jijini kwa pipa.
Msafara wa Simba katikati ya jiji la Mwanza hapa ni barabara ya Nyerere.
Ziara ya Simba imeanza leo jijini
Mwanza ambapo kesho (jumamosi) timu hiyo itashuka dimbani kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Toto Africans, kisha mara baada ya hapo siku ya jumapili Simba watakuwa Shinyanga ambapo shughuli itaanza kwa Kombe la Ubingwa kutembezwa tena katika mitaa mbalimbali mjini humo kisha baadaye jioni siku hiyo hiyo Simba itashuka dimbani uwanja wa Kambarage kucheza na mabingwa wa Uganda, The Express.
Wapenzi wa soka kanda ya ziwa hii si ya kukosa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.