Mshambulizi Cristiano Ronaldo aliwaridhisha mashabiki wa Ureno
kwa kucheza vizuri sana usiku wa Alhamisi, na juhudi zake kuiwezesha nchi yake
kuishinda Jamhuri ya Czech bao 1-0 katika mechi ya mwanzo ya robo fainali ya
Euro 2012, na kufanikiwa kuifikisha hadi nusu fainali.
Ronaldo, ambaye alifunga magoli mawili wakati katika mechi ya awali ya mashindano hayo nchi yako ilipocheza na Uholanzi, aliweza kugonga mwamba katika nusu ya kwanza na ya pili katika mechi dhidi ya Jamhuri ya Czech.
Ureno sasa itakutana aidha na Uhispania au Ufaransa katika juhudi za kufuzu kwa fainali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.