Mpambano huo wa ubingwa wa taifa wa TPBO uzito wa midle na unaosimamiwa na TPBO chini ya rais wake Yasin Abdallah na katibu mkuu Ibrahim Kamwe umemalizika vizuri na mabondia wote wapo katika hali nzuri na tayari kwa fight.
Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na Ibrahim kamwe na kueleza kuwa mabondia hao wote wawili kwa pamoja wamepata @kilo 71 na watacheza raundi kumi.
Pia kutakuwa na
mapambano ya utangulizi kama ifuatavyo;
Juma Fundi (52kg) v/s shaban
madilu (49.5kg) - watacheza raundi nane
Mohamed Shaban'ndonga' (61kg) vs Musa
hassan (61kgs) - watacheza raundi sita
Jonas godfrey (61.5kgs) vs Venance
mponji(59kg) - watacheza raundi sita
Abdalah mohamed'prince naseem'(64kgs) vs
Yohana Mathayo(65.5kgs)- raundi sita
Nasoro Hatibu 55kg vs Abdul Athuman
55kgs -watacheza raundi nne
Martin Richard 50kgs vs Hassan Kadenge 49kgs
-watacheza raundi nne
Ngumi zitaanza kama kawaida kuanzia saa kumi jioni, na tunarudia tena kusema katika ngumi hakuna kupendelea na TPBO itasimamia kwa haki zote bila kuangalia mtu. tutakachoangalia ni mchezo kuchezwa kwa kanuni za ngumi na utoaji points kulingana na bondia anavyoscore kwa ngumi halali sio kulingana na makelele ya washabiki.
Wako
IBRAHIM ABBAS KAMWE-BigRight
Katibu Mkuu TPBO
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.