Video diwani Mabula.
Akipokea msaada huo mwenyekiti wa mtaa wa Shadi, Anthony Mabasi amempongeza diwani huyo kwa kujibidiisha hadi kufanikiwa kulitatua tatizo hilo lililokuwa likikikabili kijiji chake na kuahidi kushirikiana na watumishi wa zahanati hiyo kuitunza Ambullance hiyo ili iweze kutoa huduma kwa muda mrefu.
Diwani wa kata ya Mkolani Stanslaus Mabula akijaribu Ambulance hiyo ya magurudumu matatu huku akiwa amembeba mwanakijiji wa Shadi aliyehudhuria makabidhiano hayo.
Changamoto kubwa kwa Zahanati hiyo ilikuwa ni pale ilipokuwa ikipata wagonjwa wakiwemo wanawake wajawazito kufikishwa katika hospitali hiyo hasa nyakati za usiku huku wengine wakihitaji kupelekwa kwenye hospitali ya wilaya iliyoko Butimba umbali wa km 14 kupata tiba zaidi ambazo haziwezi kutatuliwa kwenye zahanati hiyo wengi walikuwa wakipoteza uhai kwa kukosa usafiri.
Pamoja na kukabidhi Ambulance hiyo ya magurudumu matatu pia diwani huyo ametoa msaada wa mabenchi mawili madhubuti kwaajili ya watu wanao hudhuria kituo hicho cha afya.
Picha ya pamoja.
Kutokana na msaada huo wagonjwa wote wakiwemo wajawazito watarahisishiwa kupata huduma ya usafiri bure iwapo wataamriwa kupelekwa hospitali ya wilaya kupata tiba zaidi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.