ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 10, 2023

HALMASHAURI YA CHALINZE YAIBUKA KINARA WA KWANZA YAPATA NGAO YA UTAWALA BORA NCHI NZIMA

 VICTOR MASANGU/PWANI

 BARAZA LA MADIWANI NOVEMBA 9/2023.

Katika kutambua mchango na jitihada kubwa zinazofanywa na Halmashauri mbalimbali nchini, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeitunuku Ngao ya Ushindi wa Kwanza wa Tuzo ya Uutawala Bora, na matumizi mazuri ya fedha za Serikali kutokana na kukidhi vigezo vilivyowekwa.. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze HASSANI MWINYIKONDO wakati wa kikao cha Baraza la madiwani cha robo ya kwanza kwa kipindi cha kuanzia mwezi julai hadi Septemba mwaka 2023/2024.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo RAMADHAN POSS amebainisha kwamba mafanikio ambayo wameyapata kuibuka kidedea katika shindano hilo la utawala bora ni kutokana na kufanya kazi kwa ushirikiano na watumishi wa idara zote.


Naye  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halma Okash amewataka madiwani na watendaji kuwabana baadhi ya watu ambao wanakwepa kulipa kodi ya serikali kwa makusudi.


SIJALI MPWIMBWI,OMARY MSONDE NA TUNU MPWIIMBWI Ni madiwani wa Halmashauri ya Chalinze.

Halmashauri ya Chalinze iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani imeweza kuibuka kidedea na kupata tuzo hiyo ya utawala bora na kuwa ya kwanza katika halmashauri 184 nchi nzima.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.