ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 5, 2018

BENKI YA KCB TANZANIA YANDAA SEMINA ‘BIASHARA CLUB’ KWA WAFANYA BIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME).

Bi. Lightness May, Meneja wa Mauzo ya Kibiashara wa Benki ya KCB akijibu maswali kutoka kwa wafanyabiashara wa jiji la Mwanza katika hafla ya Biashara Club Workshop iliyofanyika Gold Crest Hotel tarehe 29.11.2018 jijini Mwanza. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 ilikuwa na lengo la kutoa mafunzo katika maswala ya usimamizi wa fedha,uendeshaji wa biashara na sheria zinazohusu kodi.
Zaidi ya kutoa elimu ya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara na sheria za kodi, KCB Biashara Club 
pia inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa biashara zao kwa 

kuwakutanisha na wafanyabiashara wa nje na ndani ya nchi.



Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2017, KCB Biashara Club imeendelea 
kuonyesha dhamira yake ya kukuza biashara katika seckta ya SME kwa 

kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati 

yaani (SME) pamoja na kuwaonyesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli 
zao za kibiashara.


Semina hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza ilikusanya
wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja tofauti, wakiwa 
na changamoto mbali mbali za kibiashara zikiwemo rasilimali, ushindani, 

uelewa finyu katika maswala ya kodi na nyinginezo. Nia kubwa na 

KCB Bank ikiwa ni kutaka kuwafundisha wafanyabiashara njia bora ya 
kukabiliana na changamoto zinazowakumba.

Akiongea katika warsha hiyo, Meneja wa Tawi, KCB Bank Mwanza, Nd. 
Emmanuel Mzava aliwashukuru wafanyabiashara na wajisiriamali kwa 

kujitokeza kwa wingi kuja kupata mbinu muhimu zitakazowasaidia katika 

kukabiliana na changamoto za kibiashara. “Mtegemee semina kama 
hizi kwa siku za mbeleni kwani Mwanza ni jiji linaloonyesha kushamiri 
kibiashara” aliongezea Nd. Mzava.

Nd. Swetbert Thomas ambaye ni mtaalamu wa mswala ya kodi 
aliyealikwa na KCB Bank Tanzania mahususi kutoa mafunzo katika warsha 

hiyo aliwahimiza wafanyabiashara hao kuhusu muuhimu wa kuelewa 

mifumo ya kodi hapa nchini na ni kwa namna gani unagusa biashara 
zao.

Mbali na kufaidika na ujuzi wa mambo kupitia semina na safai mbalimbali 
zinazoandaliwa na kitengo cha “Biashara Club”, wanachama pia 

watafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao ambao 

utapelekea wao kuongeza si ujuzi wa kibiashara tu, bali pia kupanua 
wigo wa biashara zao. 

KCB Bank inatambua umuhimu wa wafanya biashara 
wadogo na wakati katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia 

inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanya biashara hao 

hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara.

Kuhusu Benki ya KCB
Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa 
mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea 

katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi 

na Ethiopia.

Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii 
ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 

15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika 

Mashariki.

Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, 
Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya 

KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua 

milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika 
kukuza sekta ya fedha nchini. 

Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania 
bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, 

Msimbazi, Lumumba, Buguruni, Oysterbay, Mbagala jijini Dar es 

Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro.


Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi 
ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea 

nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.