Breaking News!
Kikao cha baraza la madiwani Jijini Mwanza kilichokuwa kikiongozwa na yule meya aliyekamatwa na jeshi la polisi asionane na Rais (Mstahiki Meya James Bwire) kimeingia malumbano na mvutano na hata kuvurugika.
Ni takribani miezi miwili sasa hakuna kikao chochote kimeweza kuketi na kujadili namna ya kusukuma shughuli za maendeleo kwa Jimbo la Nyamagana ambako ndiko Halmashauri ya jiji la Mwanza inapatikana.
Leo imeshuhudiwa kikao hicho kuvunjika tena huku kukiwa na giza machoni mwa wananchi wasijue ni lini watapata taarifa zitakazo eleza nini kimefanyika kupitia mipango mbalimbali iliyowekwa awali na hatma kwa mipango ya baadaye..........
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.