Ajali hiyo ilitokea jana Ijumaa, Oktoba 3, majira ya saa 4:00 asubuhi katika eneo la Usa River nje kidogo ya Jiji la Arusha ambapo gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Mark X lenye namba za usajili T 796 DGF lilikuwa lilkiendeshwa na Chijana lilipoteza mwelekeo na kupinduka.
Ajali hiyo ilipelekea pia kifo cha James Alfred (40) mkazi wa Tabata ambaye ilielezwa kuwa alikuwa rafiki kipenzi wa Chijana.
Chijana, ambaye taarifa za uhakika zimesema alikuwa karani mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Kitengo cha Uhandisi, katika Bandari ya Dar es Salaam, alikuwa katika maandalizi ya mwisho kabla ya kufunga ndoa pia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alieleza kuwa ajali hiyo ilisababishwa na mwendokasi wa gari la Chijana wakati akitaka kulipita gari aina ya Toyota Noah yenye namba T841 BVQ, lililokuwa ikiendeshwa na Joseph Bandari mkazi wa Maji ya Chai, Arusha.
“Wakati David (Chijana) akijaribu kuipita Noah, mbele yake kulikuwa na lori linakuja kwa kasi, Sasa akaona ili asikutane nalo uso kwa uso, arudi kushoto. Akaigonga Noah kisha akapoteza mwelekeo na kwenda kugonga miti.” alisema Kamanda Mkumbo.
Aidha, Kamanda Mkumbo alisema watu hao walikufa papo hapo na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufani ya Mount Meru
mkoani Arusha.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.