ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 8, 2012

MHASHAMU BABA ASKOFU BALINA KWA SASA ANAAGWA JIJINI MWANZA, KUZIKWA SHINYANGA JUMAMOSI


Msafara ulioubeba mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo kuu la Shinyanga marehemu Alosius Balina ukiingia katika himaya ya Kanisa kuu la Bugando jijini Mwanza leo kwaajili ya kutoa nafasi kwa wakazi wa mkoa huu kutoa heshima zao za mwisho 

Mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo kuu la Shinyanga marehemu Alosius Balina ukishushwa toka kwenye gari tayari kufikishwa eneo maalum la ibada kanisani hapa 

Mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo kuu la Shinyanga marehemu Alosius Balina ukiingizwa ndani ya kanisa kuu la Bugando kwaajili ya ibada ya heshima za mwisho kwa wakazi wa Mwanza.

Padre wa Parokia ya Kanisa Katoliki Bugando Padre Alfred Lwamba ameongoza mapokezi ya ibada ndogo ya kupokea mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo kuu la Shinyanga marehemu Alosius Balina. 

Watu mbalimbali pamoja na watumishi wa mungu kutoka ndani na nje ya jiji hili wamehudhuria ibada hii.

Upande wa akina mama.

Upande wa akina baba.

Mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo kuu la Shinyanga marehemu Alosius Balina ukiwa tayari kwaajili ya kuagwa katika Kanisa kuu la Bugando jijini Mwanza

Kisha baada ya ibada fupi ulianza utaratibu wa waumini, masista na mapadre kutoa heshima zao za mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo kuu la Shinyanga marehemu Alosius Balina.

Heshima za mwisho zikiendelea....

Kimya kimetawala hapa, huku sauti za taratibu za uimbaji zikisikika.....

Wanavyuo waliomfahamu aliyekuwa Askofu wa jimbo kuu la Shinyanga marehemu Alosius Balina nao wamejumuika kanisani hapa.

Kanisa 

Msafara wa kutoa heshima za mwisho uko hadi nje...

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.