ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 10, 2012

MSONDO NGOMA YAKABIZIWA VYOMBO NA KONYAGI



SAID MABELA AKIPOKEA  KUTOKA KWA DAVID MGWASA










Na Mwandishi Wetu 

BENDI kongwe nchini ya Msondo Ngoma music band  imekabidhiwa vifaa vya muziki na kampuni ya Konyagi Dar es Salaam 
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Konyagi nchini, David Mgwasa alisema vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya kuenzi utamaduni wa Mtanzania na kuifanya msondo kuwa imara katika kutoa burudani kwa watanzania.

"Msondo ni bendi kongwe tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964 imesimama imara katika kutoa burudani ya uhakika kwa watanzania sanjari na kutumia nyimbo zake katika kuelimisha, kufunza jamii ya watanzania walio wengi," alisema Mgwasa.

Alisema watu wengi kwa kuwepo bedndi ya msondo wamewezakupata mafunzo mengio kupitia nyimbo zao ambazo nyingi zimekuwa zikitoa mafunzo kwa watanzania.


Hivyo alisema kuwa kwa kuwapatia vifaa hivyo, Msondo itakuwa moto wa kuotea mbali katika kutoa burudani ya uhakika hali itakayofanya bendi nyingine kwa wasindikizaji katika tasnia ya muziki wa dansi nc?hini.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Maalim Gurumo alisema kuwa kwa sasa wanadeni kwa Watanzania na kampuni ya Konyagi katika kutoa burudani ya uhakika baada ya kupatiwa vifaa hivyo.

"Tunaamini baada ya leo kupata vifaa hivyo tutatoa burudani ya uhakika sanjari na kukijenga vyema kikosi chetu kwa lengo la kukiimarisha," alisema Gurumo.

Kiongozi wa bendi hiyo Said Mabela alitoa shukrani wa kampuni ya konyagi kwa kuwapatia vifaa hivyo na kuahidi kuendelea kutoa burudani safi kwa Watanzania na Afrika kwa ujumla.

"Tunashukuru kampuni ya Konyagi kutupatia vifaa vya muziki ambavyo kwetu ilikuwa ni vigumu kwa kipindi hiki kuvipata, hivyo tunaamini tutafanya tutaendela kuwa vinara katika kutoa burudani nchini," alisema Mabela.

Ofisa Habari wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa amefurahishwa na kampuni hiyo kutoa vifaa hivyo akiamini kuwa vijana wake watafanya vizuri zaidi katika ushindanio wa muziki huo nchini.

Pia aliwaomba wadau wengine wa muziki nchini kujitokeza  kuisaidia Msondo ili kuijengea uimara katika ushindi wa muziki huo nchini ili kuendelea kuwa bendi bora na ya kuigwa nchini. 

WANAMZIKI WA BENDI YA MSONDO NGOMA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KONYAGI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.