ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 11, 2013

DALADALA YAUA ABIRIA WA PIKIPIKI IGOMA.


Askari wa usalama barabarani wakipima ajali iliyotokea leo jioni eneo la Igoma jijini Mwanza na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye anatajwa kuwa ni abiria ambaye alikuwa amembeba dereva wa pikipiki iliyopata ajali yenye namba za usajili T988 BDW ambapo dereva wake (ambaye ndiye mmiliki aliyekuwa amepakizwa) alikimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea, inasemekana kuwa pikipiki hiyo iliyokuwa kwenye mwendo kasi iligonga kwa nyuma basi la abiria aina ya daladala lenye namba za usajili T768ASA lililosimama ghafla mbele ya pikipiki hiyo kwa ajili ya kupakia abiria.

Kijana aliyefariki  alitambulika kwa jina la Mayunga Clement Lufuta.


Marehemu Mayunga Clement Lufuta.


Pikipiki hiyo yenye namba za usajili T988 BDW eneo lake la mbele limezama kabisa uvunguni mwa daladala kiasi cha kuharibika vibaya.


Baada ya trafiki kufanya upimaji gari la abiria (daladala) linalofanya safari zake Buzuruga hadi Sumve liliruhusiwa kutoka barabarani na kupaki pembeni kwaajili ya taratibu nyingine kufanyika ikiwa ni pamoja na kuuondoa mwili wa kijana huyo pamoja na pikipiki iliyopata ajali ili kupisha shughuli nyingine za usafirishaji barabarani kuendelea. 


Pikipiki iliyopata ajali ikiondoshwa barabarani kwa amri ya trafiki.


Kisha mwili wa marehemu Mayunga Clement Lufuta ukatolewa barabarani kusubiri gari maalum kupelekwa hospitali ya rufaa Bugando kuhifadhiwa.


Kujulikana kwa jina la marehemu huyo kumekuja mara baada ya askari wa usalama barabarani kumpekua na ndipo walipokuta walet yenye vitambulisho mbalimbali kikiwemo kitambulisho cha mpiga kura. 

Hiki ndicho kitambulisho kilichosaidia kumtambua marehemu.


Wananchi wakiwa wameuzunguka mwili wa Mayunga Clement Lufuta aliyepoteza uhai kwa ajali iliyotokea leo jioni majira ya saa 10:25 eneo la Igoma jijini Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.