Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza bondia Ramadhani Mbegu 'Migwede' kupiga ngumi ya Mkunjo wa chini Upcut wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Super D Coach shule ya Uhuru kariakoo Dar es salaam jana Mbegu anajiandaa na mpambano wake wa julai 7 utakaofanyika katika ukumbi wa manka pub Chanika Magenge
Na Mwandishi Wetu Baada ya tamba mbalimbali za hapa na pale sasa mabondia Hussein Alli 'Gobosi' na Ramadhani Mbegu' Migwede' watazipiga julai 7 katika ukumbi wa Manka Pub Chanika Magenge mpambano wa raundi 8
Migwede amea wa ahidi mashabiki zake kuja kwa wingi kwani anacheza katika uwanja wa nyumbani na ato waangusha mashabiki zake ujue nimekuwa nikikimbiwa na mabondia mbalimbali hivyo bondia yoyote anaekuja katika anga zangu nakanyaga tu anakuwa kama ngazi
Mpambano uho ulio andaliwa na Rajabu Mhamila 'Super D' kupitia kampuni ya Super D boxing Promotion amesema kuwa pambano hili ndio litakalo amua nani zaidi bada ya mabondia hawo kuwa na viwango sawa kwa sawa Ambapo katika viwango vya ubora nchini Tanzania Mbegu yeye ni nambari 10 wakati Hussein Ally yeye ni namba 14 katika ubora
Super D aliongeza kwa kusema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ambapo Hamidu Kwata atazipiga na Luckman Ramadhani na Salum Mandai 'Pacho' atazidunda na Waziri Rosta wakati Juma Zingiziwa ataoneshana umwamba na Alex Kachelewa juma Malenda atavaana na Ibrahimu Makubi na Hussein Shemdoe atazipiga na Juma Kadoda wakati Said Mbelwa atazidunda na Shabni Kaoneka na mapambano mengine mbalimbali ya vijana chipkizi
Super D aliendelea kwa kuseka kuwa siku hiyo ngumi zitaanza mapema sana kutokana na kuwa na mapambano mengi na makali hivyo kuwataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuwai kufika ukumbini ili ngumi zianze kwa wakati
usalamab wa mali zao ni wakutosha kabisa kwani mashabiki wanatakiwa waje na familia zao wapate burudani ya mchezo wa masumbwi |
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.