ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 24, 2012

LAKAIRO HOTEL YAADHIMISHA MIAKA 10 KWA JAMII YATOA MISAADA VITUO VYA WATOTO YATIMA MWANZA

Mwenyekiti wa Makampuni ya Lakairo Investiment Mh. Lameck Airo ambaye ni mbunge wa Rolya akikabidhi msaada wa mchele, mafuta, sukari na mashuka kwa mwakilishi wa kituo cha watoto yatima cha Hisani toka wilaya ya Ilemela, Frednand Fredrick.

Mwenyekiti wa Makampuni ya Lakairo Investiment Mh. Lameck Airo ambaye ni mbunge wa Rolya akikabidhi msaada wa mchele, mafuta, sukari na mashuka kwa mwakilishi wa kituo cha watoto yatima cha Fonelisco toka wilaya ya Ilemela, John Makoye.

Hawa ndiyo wafanyakazi wa Lakairo Hotel ambao kwa siku ya leo wanasherehekea maadhimisho ya miaka 10 katika huduma ya hotelia.

Uongozi wa Lakairo Hotel marafiki na wafanyakazi.

Maandamano yalianzia Hotelini kupita barabara mbalimbali jijini Mwanza kufanya usafi.

"Hivyo basi sisi kama Lakairo Hotel katika miaka 10 tunayofuraha kufurahia ukuaji wetu uonaoendana na utoaji huduma bora jijini Mwanza."

Maandamano ya maadhimisho yakipita barabara ya Makongoro kushoto bro Six na Janet wa Airtel pale kati...

Dah wadau walipendeza ile kisawasawa...

Katikati ya jiji wakichaniza....

Katika kusherehekea miaka 10 ya utoaji huduma bora kama taasisi Lakairo Hotel imeamua kurejesha japo sehemu ya faida yake kwa kushiriki maandamano ya shughuli za usafi wa jiji kama ilivyo kwamba ni jukumu la kila mmoja vilevile kusaidia watoto yatima na waishio katika mazingira magumu.

Kila mdau alichukuwa mtoto mmoja na kukaa nae, kuzungumza nae kwa karibu almuradi kumpa malezi ya karibu kama mzazi.

"Si unaona picha tuliyopiga sasa naiweka kwenye face book"

Ni mmoja tu aliyestukia flash hii Dj Paty left.

Kisha muzikiiii....

Ulipigwa mpambano wa kudance kati ya watoto waishio mazingira magumu na wafanyakazi wa Lakairo Hotel viduku vilifumukajeee....

Mama mwenyekiti akiwa katika tabasamu na mtoto wake wa sherehe.

Kulia ni meneja Lakairo Hotel na kulia ni mkurugenzi Dany Lameck wakiwa na watoto wa sherehe, hakika ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa watoto hawa yatima.

Picha ya pamoja kila mdau na mtoto wake wa sherehe aliye mchaguwa.

Kisha chakula kizuri meza kwa kila mmoja...

Nilisahau kukwambia washindi katika kudansi mangoma walikuwa watoto yatima ambao waliifunika ile mbaya timu ya wafanyakazi Lakairo Hotel.

Tupe maoni yako

5 comments:

  1. Hongera Lakairo Hotel kwani miaka kumi si mchezo

    ReplyDelete
  2. Happy birthday Lakairo hotel mwanza

    ReplyDelete
  3. Ni jambo zuri la kuigwa na jamii yote ya watanzania wenye mali na wasio na mali ila tu tahadhari kwa hao wamiliki wa vituo wasitumie watoto hao kama mitaji ya kujinufaisha wao nilifurahi sana pale Six alipokaribishwa na wewe bro na kusema pesa iliyochangwa itakwenda kununuliwa chakula halafu kugawiwa kwa vituo hivyo viwili, safi sana ni wazo chanya.
    big up lakairo hotel

    ReplyDelete
  4. Si mchezo nilishuhudia kwenye televisheni ya BARMEDAS.TV, Katika wamiliki wa mahotel huyu Jamaa ni wa kwanza kwa Tanzania nzima. Watoto yatima na wale waishio mazingira magumu pia ni watoto wa wazazi walio hai. AFRIKA ITAJENGWA NA WAAFRIKA WENYEWE, TUSITEGEMEE PESA ZA WAZUNGU KULEA WATOTO WETU KWANI HATA WAO WANAJITOLEA KAMA ALIVYOFANYA MZEE LAKAIRO WA MWANZA. MUNGU AKUBARIKI DANIEL LAMECK MKURUGENZI WA LAKAIRO PAMOJA NA MWENYEKITI MH. LAMECK AIRO. TUNASHUKURU SANA WATANZANIA KWA MOYO HUO.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.