ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 22, 2012

VITU ADIMU SOKO LA SAMAKI MWALONI KIRUMBA

UTALII TANZANIA SI MBUGA ZA WANYAMA TU..Samaki aina ya Sangara tayari kwa kukatwakatwa vipande soko la kimataifa Mwaloni kirumba jijini Mwanza.

Wafanyabiashara wakipanga vichwa vya samaki vilivyokaushwa almaarufu 'Mapanki' kwaajili ya kufungwa marobota kwa biashara nchi za afrika mashariki na kati.

Mapanki katika mpangilio madhubuti....

Kayabo ni samaki aina ya sangara aliyesindikwa kwa chumvi nyingi maarufu sana na soko kubwa liko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako ni chakula kinacholiwa na matajiri.

Kayabo uhamishaji toka sehemu moja hadi kwenye madaraja ya viwango.

Wafanyabiashara wakichambua makayabo yaliyokauka yenye ubora yanayopaswa kuingia kwenye hatua ta uwekwaji kwenye marobota njiani kwenda sokoni.

Mwananchi akigeuza vipande vya samaki vilivyokatwa almaarufu kama 'chips' kwaajili ya kukauka vizuri juani.

Maranyingi samaki wanaosafirishwa kwa soko la nje ni minofu tu iliyokatwa kiufundi ambayo huifadhiwa kwenye makasha maalum yenye barafu, vichwa, mifupa, mikia na mabaki mengine toka viwandani hukusanywa kwaajili ya kukaushwa kama hivi kwa chakula cha walaji wengine na masalia mengine yasiyohitajika hufanywa chakula kwa kuku.

Uanikaji soko la Mwaloni Kirumba Mwanza Tanzania.

Mabaki haya ya mifupa ya samaki anikoni kwaajili ya kuchanganywa na dagaa kisha husagwa kutengenezwa kama sehemu ya chakula cha kuku.

Oda maalum ya Mwanamuziki maarufu Kongo mkongwe mwenye bahati ya kupata mialiko mingi nchini...

Wanajulikana sana kwa jina la Ndege Mwarabu wakiranda kwa makundi katika meza zilizowazi za kuanikia samaki wa biashara sokoni Mwaloni Kirumba jijini Mwanza hakika ni utalii tosha.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.