Wednesday, December 29, 2010
MICHEZO
Meneja wa Chelsea, Carlo Ancelotti, amewatonya wachezaji wake, hawana budi kuzinduka usingizini kabla matumaini yao ya kuutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya England hayajayeyuka. Chelsea walikubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Arsenal na sasa wamecheza michezo sita ya ligi bila chereko na wameporomoka hadi nafasi ya nne ya msimamo wa ligi.Ushindi wa mwisho kwa Chelsea msimu huu wa ligi, ilikuwa tarehe 10 mwezi wa Novemba dhidi ya Fulham. Alipoulizwa ni kwa muda gani mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich, ataendelea kuwa mvumilivu, Ancelotti alijibu: "Sijui. Kwa vyovyote vile hatakuwa mwenye furaha wakati huu."
Mechi za jana Manchester City ilipojisogeza hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Soka ya England kwa ushindi wa bao 4-0, wakati Mario Balotelli alifunga mabao matatu dhidi ya Aston Villa, mawili yakiwa kwa mikwaju ya penalti.
Katika game nyingine iliyovuta macho na hisia za mashabiki wengi kufahamu matokeo yake ni ile iliyochezwa baina ya Birmingham na Man U'.
Lee Bowyer wa Birmingham City alipachika bao katika dakika ya tisini na kuifanikisha klabu yake kuibana mbavu Manchester United kwa droo ya 1-1. Hata Hivyo licha ya sare hiyo United wamerejea kileleni.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.