Hali iko hivi nje ya dimba la Emirates nyumbani kwa washika bunduki Arsenal ambao leo majira ya usiku wataumana na Chelsea kiwanjani hapa, kocha Arsene Wenger akikitaka kikosi chake kupata ushindi ili kujiweka ktk nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu .
Hali ya hewa ya baridi kali inaendelea kuleta bugudha kubwa katika michezo nchini Uingereza, hasa wakati huu wa sikukuu.
Jana Michezo ya Ligi Kuu ya soka ya England kati ya Blackpool na Liverpool na kati ya Everton na Birmingham ilifutwa.
Ipswich ambao walikuwa wawakaribishe nyumbani Watford katika mechi za Championship jana, mchezo huo nao umeahirishwa, wakati mechi ya Ligi Kuu ya Scotland kati ya Kilmarnock na Dundee United nao umeahirishwa.
Michezo ya rugby, pambano baina ya Gloucester na Northampton limeahirishwa kutokana na baridi kali. Pia michezo mingine ya rugby ya ligi kuu kati ya Bath na Exeter ilifutwa na ule mpambano baina ya Newcastle dhidi ya Leeds umesogezwa mbele, badala ya kufanyika Jumapili jana, sasa utachezwa leo Jumatatu.
Katika soka tena, michezo ya Championship ya Crystal Palace, Derby, Ipswich, Scunthorpe na Middlesbrough pia ilifutwa; michezo 22 ya Ligi daraja la kwanza na la pili pia iliahirishwa. Mechi ya ligi daraja la kwanza pekee iliyochezwa jana ni kati ya Huddersfield na Hartlepool, wakati ya ligi daraja la pili, kati ya Wycombe na Hereford ulinusurika kutochezwa na hatimaye ukachezwa kama ulivyopangwa.
Chukua Mkwanja Wako Mapema Leo
-
HATIMAYE baada ya jana kushuhudia mechi kibao zikipigwa na matokeo mengine
yakiwa yakustaajibisha, leo hii ni zamu tena ya wababe wengine kibao
uwanja...
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.