ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 1, 2019

HATIMAYE TUZO YA UBORA KWA KAMUNI YA MWANZA QUALITY WINES YATINGA OFIZI ZA MKOA WA MWANZA


HATIMAYE Kampuni ya Mwanza Quality Wines mapema hii leo imekabidhi rasmi tuzo yake ya ubora kwa ushindi wa kwanza kitaifa kwa makampuni ya kati  (mid size company) kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.

 Kampuni ya Mwanza Quality Wines inayozalisha mvinyo wa matunda jamii ya Power Banana imeibuka mshindi wa jumla wa tuzo za kampuni 100 bora (Top 100 Awards) mwaka 2019/20 zinazotolewa chini ya uratibu wa kampuni ya ukaguzi wa hesabu za fedha KPMG kwa kushirikiana na Mwananchi Communications Limited (MCL).

Tuzo hizo zilitolewa Oktoba 25, 2019 jijini Dar es salaam huku mapokezi ya tuzo ya mshindi wa jumla yakifanyika Oktoba 31, 2019 katika uwanja wa ndege wa Mwanza ambapo hiyo ni hatua kubwa kwa kampuni ya Mwanza Quality Wines ambayo tuzo za mwaka 2018/19 ilishika nafasi ya 30.

Naye mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema kuwa kampuni hiyo licha ya kuupa mkoa heshima kwa kuibuka washindi, bali pia imekuwa changamoto kuona matokeo chanya ya mapinduzi ya viwanda kwa mkoa wake naye amejipanga vyema kuona makampuni mengine yakisifika kwa uzalishaji bidhaa bora katika soko la ndani na nje ya nchi. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.