Mradi huo ulioanza na magari 50 ambayo yametengenezwa kwa ajili ya majaribio hivyo yatakuwa yakitumiwa kama magari ya uchukuzi wa abiria jijini Kigali na kwingineko nchini humo.
Mkurugenzi mkuu wa Volkswagen Group ya Afrika kusini, Thomas Schäfer amebainisha kuwa magari haya yamo bado katika majaribio na kwamba yametengenezwa 40 aina ya e.Golf na kwamba malengo kwanza si kuuzwa ghali ingawa bei bado haijatangazwa.
''Magari haya hayana mpango wa kuuzwa kwa wateja kwa sasa. Tunalenga kwanza kuyafanyia majaribio na kujua yanafanya kazi vipi na ndipo tutakapowajulisha iwapo zitauzwa au la. Magari haya ni ghali ikilinganishwa na yale ya kawaida, kutokana na betri yake.
Betri peke yake ina gharimu kiasi cha dola 8000 za Kimarekani lakini umeme ukilinganishwa na mafuta ni bei nafuu.
Lakini iwapo serikali ikiwasaidia kwa kuweka sera mfano kwa kupata faida nafuu ,yamkini hali ikawa nzuri zaidi.
Angalia Uchina serikali iliazimia kwamba asilimia 25 ya magari yanayouzwa yawe yanayotumia umeme.''
Serge Iyakoze ni kiongozi wa madereva wa kampuni ya Valkswagen akihusika pia kutoa warsha kwa madereva wenza katika matumizi ta teknolojia ya magari hayo ambaye ameiambia BBC kuhusu wasiwasi au hofu kuhusu mwendo wa kimya wa magari hayo na iwapo hawatarajii kusababisha ajali za barabarani kwa watu waliozoea milio na honi za magari kuwashtua wanaotembea kwa miguu.
''Unapoelekea kupata ajali kawaida huna budi kupiga honi kwani dereva ana uwezo kuangalia kwa upana mkubwa mbele yake,kwa muda mfupi.
Dereva huwa na hisia za kujua kinachoelekea kutokea kwa wakati mfupi. Unapomuona mtu akizubaa unaweza kumpigia honi. Lakini huwezi kwenda ukipiga honi ovyo ovyo,kwani hata mpita njia anao uwezo kuona gari na unaweza pia kumwashia mataa.''
Kampuni imeeleza kuwa inalenga kupanua wigo wa kazi zake katika mataifa mengi ya Afrika .
Baada ya Rwanda, Ghana ndiyo inatarajia kufuata na hatimae kwingineko.
Wakati mataifa ya Ulaya yanalenga kufikia mwaka 2030 kuwa yamekwisha achana na magari yanayotumia mafuta, Afrika ndiyo imeanza safari ambayo hatima yake haijawa wazi ila waliozungumza na BBC wameelezea kuwa hatimae wao pia watafika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.