Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya mpanda Abel kimazi ameshindwa kutoa sababu za kutopitishwa jina la mgombea aliyeshinda kwa madai kuwa ni siri ya kikao cha chama.
Hata hivyo amedai kuwa chama cha mapinduzi kinafuata katiba kanuni na taratibu katika kufanyia maamuzi hivyo kikao kinauwezo wa kutengua au kumpitisha mgombea aliyechaguliwa na sio kigezo cha kura.
Na Adelina Kapaya, Katavi
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Irembo Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi wametishia kutokushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa madai ya kupitishwa mgombea wa ngazi ya mwenyekiti wa mtaa ambaye hakushinda kwenye kura za maoni .
Paskal kasomo ni mgombea aliyeshinda kwa kura 85 lakini jina lililopitishwa ni David sanganzila aliyepata kula 51na kupewa nafasi ya kugombea.
Kwa upande wake paskal kasomo ambaye alistahili kutetea nafasi hio amesema kuwa hajui sababu zilizofanya jina lake kutopitishwa kwani amefuatilia ngazi ya wilaya na Mkoa lakin hajapewa majibu.
Baadhi ya wakazi wa mtaa huo wamedai kuwa mgombea aliyepitishwa kutetea nafasi hio hana Sifa ndio maana hakushinda kwenye kura za maoni licha ya kupewa nafasi hivyo wameomba kurudishiwa mgombea waliomchagua.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.