ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 28, 2019

WIKI YA 5, HAYA NDIYO MAENDELEO YA AHADI YA JPM UJENZI WA JENGO LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE MWANZA


IKIWA ni wiki ya 5 sasa kwa mara nyingine Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo hilo linalokadiriwa kugharimu Bilioni 12 hadi kukamilika kwake mwezi Aprili, 2020.

Kwa sasa hatua ya awali ya ujenzi wa msingi umefikia asilimia 60 ambapo kazi inafanyika usiku na mchana ili kufikia malengo ya kukamilika ndani ya miezi sita badala ya miezi 12 kama ilivyopangwa hapo awali.

Hatua ya ujenzi wa jengo hilo jipya na la kisasa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilolitoa Julai 15, 2019 wakazi akizindua miradi ya afya katika Hospitali ya Rufaa Bugando ambapo Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela nazo zinachangia shilingi bilioni nne kwenye ujenzi huo.

Mradi huo unasimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza kwa kushirikiana na Wataalam kutoka Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela kupitia mfumo wa "Force Account".












Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.