ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 16, 2011

RAHA YA SOKA LA MCHANGANI MAVETERANI WA IGOMA WAFUNGWA MDOMO NA KILIMO SPORTS CLUB.

Michuano ya YANGE CUP inayoshirikisha mitaa mitatu maarufu katika kata ya Igoma wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza imemalizika jana katika viwanja vya shule ya msingi Igoma kwa mchezo kati ya Maveterani wa Igoma waliokunjugwa bila ya huruma na watoto wao timu ya Kilimo Sport Club bao 6-1.Mchezo huo ulikuwa na vihusishi, vileta raha vyenye asili ya udiferenti vilivyonifanya nikodoe macho kuuangalia mchezo kwa dakika zote tisini.

Jiografia ya Uwanja wa shule ya msingi Igoma inadhihirisha kweli naam hapa ni Rock City kwani kuna vilima vya mawe vya hapa na pale tena vipo katikati ya dimba (cheki mishale) nachakufurahisha zaidi ni kwamba ingawa wachezaji wengine walikuwa wakicheza peku lakini hakuna hata mmoja aliye jikwaa

Bao pekee la maveterani liliwekwa kimiani kupitia mkwaju wa penati iliyopigwa kiufundi naye mzee Aboubakari Balinguna. Mawe kama kawa (tizama mshale)

Mzee Kazi Mashilingi alivunja rekodi kwani alikuwemo ndani ya mchezo kwa muda wa dk 50 yaani dk 45 kipindi cha kwanza na 5 kipindi cha pili bila kuugusa mpira, hapa akitoka kufanya mabadiliko kwa timu yake ya maveterani.

Katika mchezo huo wachezaji waliruhusiwa kutoka na kuingia bila kizuizi cha idadi maalum. Lengo la michuano hiyo ni kuhamasisha mazoezi kwa wazee ili kuimarisha afya.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.