ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 9, 2025

RAS LINDI:BIL7.8 ZA MTAMA ZIKAMILISHE UJENZI WA SHULE KWA WAKATI

Katibu Tawla Mkoa wa Lindi Zuwena Omari ametoa wito kwa Menejimenti ya Halmashauri ya wilaya ya Mtama kuhakikisha wanafunzi wote waliopangiwa na kaundikishwa wanaripoti shule kwa wakati na wanakimilisha ujenzi wa shule kwa muda uliopangwa. 

Na Fredy Mgunda, Lindi.

Wito huo ameutoa leo alipotembelea halmashauri hiyo kuona maandalizi ya uripoti wa wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza na ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa shule zenye thamani ya Bil 7.8. 

Akizungumza mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtama, watalaamu wa halmashauri, Kamati za ujenzi na wawakilishi wa wananchi amesema , halmashauri imepata fedha nyingi ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anasimamia vema fedha hizo.

“Wito wangu kwa viongozi wa Halmashauri ya Mtama, wakati wote tunapopokea fedha za miradi tuwe tayari kutekeleza na kimsingi serikali imekuwa ikileta fedha za miradi ya maendeleo kila mwaka kwa ajili ya miradi tofauti tupokee fedha hizi tupange utekelezaji na tuwe na usimamizi wa mara kwa mara tuhakikishe ubora na umalizikaji kwa wakati, Mkurugenzi hili ni lakwako kuhakikisha kwamba basi muda tuliokubaliana na wakandarasi wetu miradi hiyo inakamilika kwa wakati “ Zuwena Omari Katibu Tawala Mkoa Lindi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtama Anderson D Msumba amesema wanamshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi kwa mara kwanza kupata fedha hizo na amemuahkikishia Katibu Tawala Mkoa kukamilisha miradi mwezi wa Nne mwishoni.

Mwakilishi wa wenyeviti wa kutoka Halmashauri ya Mtama Juma Omari Salumu wa kijiji cha Kiwalala amemshukuru Mhe. Rais kwa mradi huo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi na viongozi wote.

Brigita John Mponda mkazi wa kijiji hicho kwaniaba ya wananchi amesema miradi hiyo wameipokea vizuri miradi  ujenzi wa shule mpya kwani inakwenda kuwaletea elimu bora kwa watoto wao.

Bil 7.8 ya halmashauri ya Mtama inakwenda kujenga shule ya wavulana kanda ya kiwalala, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu 6 ya choo shule ya msingi Mahumbika, Ujenzi wa Shule ya mpya ya Msingi –Mtakuja Nyangao, Ujenzi wa Madarasa 5 Shule ya Msingi Simama, Ujenzi wa shule ya sekondari Mtakuja kata ya Nyangao, Ujenzi wa shule mpya ya Amali Mkoa na Ujenzi wa shule ya Sekondari kata ya Pangani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.