MWANDISHI:- VICTOR MASANGU, PWANI
IMESOMWA NA ALBERT G.SENGO
Zaidi ya wananchi wapatao laki mbili kutoka maeneo ya kata za Msoga pamoja na Msata Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani hatimaye wameondokana na kilio cha muda mrefu cha kuwepo kwa changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama baada ya kukamilika kwa miradi mipya ya visima pamoja na ujenzi wa tenki kubwa la maji lenye uwezo wa kujaza lita zaidi ya milioni 2.
Baadhi ya wananchi Wilayani Bagamoyo hususan wakinamama wakizungumza katika nyakati tofauti wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa maji Mhandisi kundo Methew ya kutembelea miradi mbali mbali hawakusita kumshukuru kwa dhati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwakomboa na kuwatua ndoo kichwani kwani hapo awali walikuwa wanateseka kutembea umbari mrefu kwa ajili ya kufuata huduma ya maji.
Naibu Waziri wa maji Mhandisi Kundo Methew amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani yenye lengo la kuweza kutembelea miradi mbali mbali ambayo inatekelezwa na Dawasa pamoja na Ruwasa ikiwa pamoja naa kusikiliza kero na changamoto kutoka kwa wataalamu ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.