ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 25, 2012

WAZIRI NAGU MGENI RASMI KONGAMANO LA MAKATIBU MUHTASI LITAKALOFANYIKA MALAIKA HOTEL MWANZA TRH 27 NA 28 APRIL 2012

Mwenyekiti wa TAPSEA Pilly Mpenda kulia akiongea leo na waandishi wa habari (hawapo pichani) anayefuata ni Mkuu wa Idara ya Uhazili TPSC Agatha Wanderage na Judith Nguli ambaye ni Mratibu wa Mafunzo ya Uhazili TPSC.
Chama cha Makatibu Muhtasi Nchini (Tanzania Personal Secretaries Association TAPSEA) kitaendesha kongamano la siku mbili katika Hotel ya Kimataifa ya Malaika, iliyo nje kidogo ya jiji la Mwanza tarehe 27 na 28 Aprili 2012.

Kongamano la jijini Mwanza ni la pili kuratibiwa na TAPSEA baada ya komngamano la Kwanza kufanyika Jijini Arusha, mwezi Mei, 2011, ambalo pia liliambatana na uzinduzi rasmi wa Chama.

Kongamano hilo linatarajia kuwakutanisha makatibu muhtasi zaidi ya 1,500 kutoka Wizara na Asasi za Serikali, Halmashauri na kampuni za kutoka sekta binafsi, kote nchini na linatarajiwa kufunguliwa Rasmi na Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji, Mhe. Dk. Mary Nagu (MB), ambaye ndiye ni muasisi wa wazo la kuunda chama hiki.

Lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha makatibu muhtasi kutoka kote nchini ili kuwapatia mafunzo ya kupanua uelewa wa masuala yanayohusu fani ya ukatibu muhtasi na namna fani hiyo inavyoweza kuboreshwa kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na mwingiliano ba maendeleo ya upashanaji habari yanayoletwa na utandawazi na teknolojia ya habari na mawasiliano.

Aidha, kongamano hilo linalenga kuwapatia makatibu muhtasi fursa ya kukumbushana kuhusu miiko na maadili ya fani ya uhazili na kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Makatibu Muhtasi pia watawasilisha na kujadili ufumbuzi wa kero mbalimbali zinazowakabili katika utendaji kazi wao wa kila siku.

BAADHI YA MAFUNZO YATAKAYO TOLEWA
1. Katibu Muhtasi kama chachu ya mabadiliko katika utendaji wa utumishi wa Umma.
2. Ufahamu kuhusu ugonjwa wa Fistula, Athari zake na Matibabu yake.
3. Ufahamu kuhusu kansa za matiti na shingo ya kizazi.
4. Stadi za Mawasiliano na Mahusiano ya Umma kwa Makatibu muhtasi.
5. TAPSEA kama chombo cha Mabadiliko kwa Makatibu muhtasi.
6. Fursa Mbalimbali kwa Makatibu Muhtasi za kujiendeleza kitaaluma na kimaadili.

Wadhamini wa kongamano hilo ni Sahara Communication, Nyanza Bottlers, Serengeti Breweries, Mamlaka ya Bandari, Clouds FM, PSPF, NSSF, EWURA, Tanzania Private Sector Foundation, METRO, Barmedas, Gold Crest Hotel, Isamilo Lodge, Mukesh Travel, Dar Lux, Malaika Beach Resort, TAI FIVE HOTEL, MAC PHOTO SPOT, 540 na Precision Air.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.