Akiongea katika hafla ya makabithiano Afisa uhusiano wa Airtel T Afisa mauzo kanda ya kati bw Hillary Tarimo alisema" Airtel kwa kupitia programme ya shule yetu imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule nyingi nchini Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya shule za sekondari wilayani Kondoa na kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa shule zitakazokabithiwa. Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani tunatambua elimu ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya kesho. Aliongeza
Tarimo.
Afisa mauzo wa Airtel kanda ya kati bw Hillary Tarimo akimkabithi vitabu vya taaluma bwana Ibrahim Juma Mwesi Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Itaswi katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya Sekondari Gubali ambapo Airtel kupitia programme ya shule yetu imegawa vitabu kwa shule za sekondari nne ziliziko wilaya ya kondoab mkoa wa Dodoma, shule zilizopatiwa vitabu ni pamoja na Goma,Hurui, Gubali na Itaswi, akishuhudia katika ni Kessy Musilenga Kessy Makamu mkuu wa shule ya Sekendari Gubali
Naye Makamu mkuu wa shule ya sekondari Galibu Bw Kessy Musilenga alisema" nachukua fulsa hii kuwashukuru Airtel kwa kutufikia na kutoa msaada wa vitabu kwa shule zetu na kupunguza changamoto zilizokuwepo katika shule hizi, tunayofuraha kwa shule yetu na wenzetu wa shule za jirani zilizopo wilayani kondoa kupata nyenzo muhimu ambazo zitainua kiwango cha elimu kwa wakazi na wanafunzi wa wilayani" Tunawaasa wanafunzi kuvitumia vizuri vitabu hivyo ili vilete matokeo vizuri kwa wanafunzi, Tunaamini jamii ikipata elimu bora maendeleo ya shughuli mbalimbali za uchumi yatafanyika kwa ufanisi zaidi na kuleta mafanikio makubwa kwa jamii. Aliongeza Kessy.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, siku chache zilizopita Airtel ilitoa msaada wa computer 20 na vitabu vyenye thamani ya million 10 kwa chuo kikuu cha Dodoma - UDOM hii ni katika kurudisha faida inayoipata na kuchangia katika huduma kwa jamii.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.