ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 3, 2013

MDAHALO WA WADAU WA MAENDELEO YA MKOA WA MWANZA HIII LEO

Fanuel Yona akiongoza mada kuhusu fursa za uwekezaji mkoa wa Mwanza katika mdahalo wa wadau wa maendeleo ya mkoa wa Mwanza uliofanyika katika ukumbi wa Gold Crest. 

Mada kuhusu dhana na uzoefu wa Public private partnership na mipango ya muda mrefu nayo iliwasilishwa.

Wadau nao walipata fursa ya kuelezea uzoefu wao na kufanya uchambuzi wa sera za uwekezaji na biashara, juu ya nini hakikpsawa, nini si sahihi na nini tunaweza kufanya.

Wadau wa habari kwenye mdahalo huo.

Uchangiaji.

Wadau wakihifadhi masuala muhimu ya Mdahalo.

Safu ya waandishi wa habari kutoka kulia ni Flora Magabe, Grace Chilongola wa Habari Leo, George Ramadhan wa gazeti la Nipashe na Erika Elias wa RFA

Afisa habari wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Joseph Mlinzi akizibainisha fursa za uwekezaji zilizopo katika jiji la Mwanza.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara Mwanza TTCIA Bwana Eribariki Mmary amesema kuwa bado hali ya ufanyaji biashara nchini si ya kuridhisha kwasababu watu wengi wamejitumbukiza katika ufanyaji biashara pasipo kujua taratibu za kufanya biashara kutokana na kuigana, wengi hawafanyi uchunguzi kwa biashara wanazo anzisha.



Wadau wakijishughulisha katika kunakili masuala muhimu.

Rais wa Klabu za waandishi wa Habari nchini Keneth Simbaya kwa upande wake alisema kuwa watanzania wengi kwa sasa wanatumia muda mwingi kujadili matatizo bila kutafuta ufumbuzi hawajui kuwa kadiri wanavyotumia muda mwingi kujadili matatizo wanafifisha uono wa kupata mawazo ya kufumbua matatizo.

Hivyo amewataka kubadilika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.