ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 31, 2023

WATU 35 WAFARIKI BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA INDIA

 


Takriban watu 35 wamefariki baada ya kutumbukia kwenye kisima walipokuwa wakisali katika hekalu moja katika jimbo la kati la India la Madhya Pradesh.

Wengine 14 wameokolewa na mtu mmoja bado hajapatikana katika ajali hiyo iliyotokea katika mji wa Indore.

Polisi wanasema waathiriwa walikuwa wamesimama kwenye slab ya zege juu ya kisima kilipoporomoka chini ya uzani wao.

Kisa hicho kilitokea siku ya Alhamisi wakati wa hafla ya maombi iliyoandaliwa katika hekalu la Beleshwar Mahadev Jhulelal kwenye hafla ya sherehe ya Kihindu ya Ram Navami.

Umati mkubwa wa waumini walikuwa wamesimama kwenye slab ya zege iliyofunika kisima ambacho kiliporomoka kwa uzito wao, na kuwatumbukiza watu wengi kwenye kisima chenye kina cha futi 40 (12m).

Vyombo vya habari vya eneo hilo viliripoti kwamba hekalu hilo lilijengwa baada ya kisima hicho kufunikwa takriban miongo minne iliyopita.

Afisa mkuu Illayaraja T amesema kuwa watu 18 walilazwamekatika hospitali hiyo baada ya kuokolewa na watu wawili wameruhusiwa .

Aliongeza kuwa msako bado unaendelea ili kumpata mtu aliyetoweka.

Timu ya wafanyakazi 75, ikiwa ni pamoja na wale wa serikali na vikosi vya kitaifa vya kukabiliana na maafa wanashiriki katika juhudi za uokoaji.

Waziri Mkuu Shivraj Singh Chouhan ametangaza fidia ya rupia 500,000 ambayo ni sawa na shilingi shilingi 13,978,185kwa jamaa wa marehemu na rupia 50,000 ambayo ni sawa na shikingi za kitanzania 1,421,998 kwa waliojeruhiwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.