Mvua za masika ambazo zimeanza kunyesha hivi karibuni Wilayani Malinyi leo Machi 28 imesababisha adha kwa watumiaji wa Barabara Kuu kutoka Malinyi kuelekea wilaya jirani za Kilombero na Ulanga.
Maji yamezingira Barabara kwa TAKRIBANI masaa sita ambapo watumiaji wa Barabara hiyo ikibidi kuchukua tahadhari kubwa kutokana na maji kukatiza Barabara ambayo inamilikiwa na wakala wa barabara nchini TANROADS.Eneo la Madumba lenye makazi ya watu pia limeathiriwa na Mvua ambayo ilinyesha usiku wa Machi 27 ambapo kujaa kwa mto Furua ulisababisha kumwaga maji katika maeneo mbalimbali ya eneo la Madumba.
Mkuu wa wilaya ya Malinyi Sebastian Waryuba amezuru eneo hilo na kushuhudia baadhi ya nyumba zikiwa zimezungukwa na maji ambapo pia kanisa katoliki Malinyi ambalo kuna shule ya wavulana ya Myakatifu Pio iliathiriwa na maji ambayo yalizingira shule na kanisa hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.