Polisi nchini Uganda wanachunguza kisa ambapo wanaume wanne wanadaiwa kumuua dada yao kwa kumpiga katika Wilaya ya Rukiga, Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.
Christine Kiconco mwenye umri wa miaka 41 anaripotiwa kuuawa
na kaka zake - Innocent Tumwekwase, Samuel Atuhirwe, Christopher Bikorwomuhangi
na Justus Mayumba - kufuatia mzozo wa ardhi.
Msemaji wa polisi wa eneo la Kigezi Elly Maate anasema kuwa
uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa familia hiyo ilikuwa na mzozo mrefu kuhusu
shamba walilorithi kutoka kwa mababu.
Kwa mujibu wa polisi, kaka hao wanne walipewa vipande vyao
vya ardhi lakini wakavipiga mnada punde tu vilipofika katika umiliki wao.
Polisi wanasema kuwa wanne hao walianza kuwaandama dada zao
wakitaka ardhi waliyopewa wasichana wa familia hiyo na sasa hilo limeishia
katika mauti.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.