ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 24, 2018

NI JOHN BOCCO MCHEZAJI BORA LIGI KUU TANZANIA BARA 2017/18

USIKU WA KUAMKIA LEO:- Mshambuliaji wa klabu ya Simba, John Bocco, (wa pili kutoka kulia) ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18.

Bocco ametwaa tuzo hiyo huku akiwapiku wachezaji wenzake beki Erasto Nyoni na Emmanuel Okwi ambao pia walikuwa kwenye kinyang'anyiro.

Ukiachana na tuzo ya mchezaji bora VPL, Bocco ambaye ni Nahodha wa kikosi cha Simba amekuwa na msimu mzuri kwa kufanikiwa kubeba pia tuzo ya Mo akiwa mchezaji bora ndani ya timu hiyo.

Vodacom ambao ni wadhamini wakuu wa ligi wamempatia kitita sha shilingi milioni 12 Bocco kama zawadi kutokana na kitengo cha kinyang'anyiro alichokuwa amewekwa.

Okwi ambaye ameshindwa katika kitengo hicho, ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kwa kufikisha idadi ya mabao 17 aliyofunga sambamba na zawadi ya shilingi milioni 3.

Aidha, timu bingwa ambayo ni Simba imepokea kitita cha fedha, shilingi milioni 96 huku Azam ambao ni washindi wa pili wakibeba milioni 48 na Yanga waliomaliza msimu wakiwa namba 3 wakijinyakulia milioni 27.

Wachezaji waliounda kikosi bora cha msimu wa 2017/18 katika Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara.

1. Aishi Manula
2. Hassan Kessy
3. Shafiq Batambuzi
4. Erasto Nyoni
5. Kelvin Yondani
6. Patrick Tshishimbi
7. Shiza Kichuya
8. Tafadzwa kotinyu
9. John Bocco
10. Emanuel Okwi
11. Marcel Kaheza

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.