ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 28, 2011

WAZIRI MKUU WA TUNISIA AJIUZULU.

Waziri mkuu wa Tunisia Mohammed Ghannouchi ametangaza kupitia televisheni ya taifa kuwa anajiuzulu- matakwa muhimu kutoka kwa waandamanaji.

Bw Ghannouchi mwenye umri wa miaka 69, anaonekana kuwa karibu sana na aliyekuwa Rais Zine al-Abidine Ben Ali tangu mwaka 1989, aliyeondoshwa madarakani mwezi uliopita.

Alisema, " Baada ya kutafakari kwa zaidi ya wiki moja, nikaanza kushawishika, na familia yangu iliniunga mkono, na hivyo kuamua kujiuzulu. Si kwamba nakimbia majukumu yangu; nimekuwa nikitimiza wajibu wangu tangu Januari 14." " Siko tayari kuwa mtu anayechukua uamuzi utakaoishia kusababisha vifo." "Kujiuzulu huku kutasaidia Tunisa, mapinduzi pamoja na maendeleo ya siku za usoni za Tunisia." Alisema.

Baada ya saa kadhaa mbadala wa Bw Ghannouchi alitajwa- Beji Caid Essebsi, mwenye umri wa miaka 84, ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya nje katika serikali ya marehemu Rais Habib Bourguiba.


Awali, polisi mjini Tunis walirusha mabomu ya kutoa machozi na risasi za onyo kutawanya maandamano ya hivi karibuni wakitoa wito wa kutaka serikali mpya na katiba mpya katika siku ya tatu ya ghasia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.